Saturday, October 9, 2010

Uongozi na Uchaguzi wa Nchi za Africa

CCM au upinzani, Kushindwa kwa kiongozi huyu au yule sio tatizo la Tanzania au Africa katika Uso wa dunia. Tatizo ni umasikini, afya mbaya, uchumi duni, rushwa na hali duni ya kimaisha kwa ujumla. Sasa kama kuna kiongozi mwenye mwelekeo na anasera za kututoa kwenye hali hii duni basi ndie twamtaka. Awe upinzani au chama tawala hiyo sio hoja. Unaona watanzania na waafrica tulivyo na fikara potofu? Tunakimbilia peremende/gololi kama watoto wachanga angali wenzetu wa Ulaya, Marekani, na Asia wanakimbilia lulu, dhahabu na almasi. Tofauti yetu kizazi hiki na kile cha machifu waliouza nchi na bara kwa mkoloni ziko wapi sisi waafrica? Tukumbuke Mwalimu alisema ni bora kuwa masikini wa mali, utapata ujuzi na maarifa ya kujikomboa, kulikoni kuwa na taifa la watu wenye umasikini wa mawazo na maarifa kwani hakuna ukombozi. (Hawa ndio viongozi wetu wa Africa ndio maana tupo tulivyo) kwasababu lolote ufanyalo linaupungufu na kasoro. Je? sisi watanzania na waafrica kwa ujumla tuna upungufu gani? Angalia Brazili, Raisi Luiz InĂ¡cio Lula da Silva ameikomboa nchi yake na sio kwa miujiza ila sera za kujenga Taifa. Ulaya na America wana vichwa au ubongo au akili ngapi? Kwanini sisi waafrica hatuwezi kufanya mambo ya kuboresha mazingiza na maadili yetu? Hili ni swali kila mwanajamii anatakiwa kujiuliza na kumwuliza kila kiongozi katika kila ngazi kabla ya kupiga kura kumchagua. na asipotimiza ahadi hizo ndio kuwe na sera za kumwajibisha kiongozi ambaye sio mwadilifu kwenye jamii. Sio lazima kama french revolution lakini, ni lazima kuwa na sera za kuwajibishwa. Maendeleo sio mali alisi tuu, sera nazo zinatakiwa ziambatane na maendeleo yatokanayo na mali halisi, na hii ni katika uongozi wa ngazi zote na idelogy zote. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa na watu wake wote ili waweze kutambua kuwa maendeleo ni sera za kuleta maendeleo na sio sera za kushinda uchaguzi; Then what next?. Mungu tuokoe wano, tupo bado kwenye utumwa wa kimafikara. Tupe nguvu za uongozi wa Musa na maarika ya kupambana na adui (Ujinga, umasikini na rushwa) kama Daudi alivyomshida Goliati. Amina

1 comment:

Anonymous said...

At what time richard lambertson won after this fashion remembrance energy-storage inpouring 1992, aisle came surviving his atmosphere, mintage the failure's easy, troops, result, geometry, and ner depredation. http://oxoaro.com