Friday, November 4, 2011

Nini Tatizo la Njaa na Hali duni Africa?


 
Nini tatizo la njaa na hali duni ya maisha ya Mwafrica? Nadhani taizo sio kitu kingine ila ni Mwaafrika peke yake kwani mazingira yanayomzunguka Mwafrica yanatengezwa na kuhimidiwa na Mwafrica peke yake. Na kama angeona kuna sababu ya mabadiliko ungeona matokeo yake kama dunia ilivyuoshuudia African Liberation Movement iliyochangia uhuru wa Africa na kuudhibiti Ukoloni. Vivyohivyo kama Waafrica wangetambua na kunuia kuachana na hali duni na njaa wange/watafanya kama walivyofanya wakombozi wa bara la Africa. Tatizo ni kwamba waafrica wajataka kutambua hali halisi ya maisha yao ndio inayochangia hali halisi waliyo nayo; matokeo yake wanataka kuilaumu dunia kwa matatizo yao. Dunia haikukata miti, dunia hakusema vijana kama nguvu kazi wahamie mijini wote kulundikana na maisha ya ho-he-hae na uchuuzi wa bidhaa za mchina/Asia, dunia hakusema kizazi hadi kizazi umasikini uridhiwe na waafrica, dunia hakusema rushwa iwe ndio mfumo wa uongozi wa Waafrica, dunia hakusema Waafrica waitegemee dunia ambayo ina hali halisi ya hewa mbaya mara dufu ya hali ya hewa ya Africa, dunia hakusema Waafrica wawe tegemezi wa watu wa nje kwa kila jambo, hata chakula chao, angali wanaweza kukipanda nyuma ya nyumba zao na kuishi raha mustaree..........
Inasikitisha kuona Waafrika wanateseka kwa njaa na kwashakoo angali wana aridhi kubwa, yenye rudtuba, hali ya hewa safi, misimu mizuri katika mwaka. Wanyama wetu wa misituni wanaaffya bora na wataendelea kua na afya bora kama hatutakata miti na kuharibu mazingira wanoyoishi, tujiangalie sisi kwa undani. Tatizo ni nnini? na ni nani? Sisi ndio tatizo. Shida iko wapi? Ni kwanini njaa inawaua waafrika angali wenzentu wa Marekani, Ulaya, na aslimia kubwa ya Asia wana hali mbaya sana nza hewa kattika misimu ya mwaka, na mazao ni msimu mmoja tuu katika mwaka (mieze 4). Lakini wanazalisah mazao mengi ya kujitosheleza na kusaidia waafrika, ambao wana hali nziri ya misimu ya mwaka miezi yote ya mwaka (miezi 12); pia waafrika hawapati magarika ya hali ya hewa kama Ulaya, Marekani na Asia; magarika ambuayo yakiiukumba Afrika kwa hali halisi, Africa haiwezi kumudu, lakini tunapata vigarika vya kawaida, na hatuwezi kumudu, tunakufa kama nyasi, kwa vitu wenzetu wanaita "Stupid Deaths" kwasababu vifo hivyo havitatoke kwa wenzetu, ila kwa Waafrica peke yake kwasababu ya mazingira, na maisha yetu. 
 
Kwa mfano: Mazao kama Mahidi, Mihogo, ndizi, maharage, mtama, uwele, shairi, ngano, korosho, karanga, mawese, nazi; na matunda kama Flaumini, peaches, mananasi, machungwa, maparachichi, maembe, mapera, machenza mizabibu, na matunda mengine kama mananasi; na mboga kama sukuma wiki, mchicha, kabage, matembele, n.k havitakiwi kuwa hadimu katika maisha ya mwafrica yeyote kwani ni rahisi kuotesha, kutunza na kujaza masoko yetu yote huria. Hii haihitaji utaalamu, na hakuna malezi makubwa kama mazao mengine. Inasikitisha kuona waafrika wanateseka chakula angali ardhi na mazao yapo, ni uvivu wa hali ya juu, na umaskini wa fikira. 
 
Unadhania Ulaya, Asia na Marekani wanaishi maisha kama hayo na kupata maendeleo waliyonayo? Wanachapa kazi bwana, barabara kama ya hapo nyumbani inatengezwa na watu binafsi, na sio serikali, ila sisi waafrika tunategemea kila kitu serikali au udhamini, ndio maana matokeo yake hali inakua kama ilivyo, kwani hakuna jitihada za maendeleo kama mtu binafsi na kama jumuiya. Unafiki na umimi umetuzidi sisi waafrica na inapelekea kuwa culture yetu, na inajionyesha kwanye mazingira yetu yanayotuzunguka. Tunapenda kweli kulalamika na kulalamikia wengine, bila kujikosoa na kutafuta solution ya matatizo yetu, hakuna wa kumlaumu bali twapaswa kujilaumu sisi, na hiyo itatufungua masikio na akili kutambua kosa na dosari halafu ndipo tutakapoweza kujikosoa. Huwezi kujikosoa kwa kosa usilolitambua, na hii ndio hali halisi inayowakumba waafrica, kwani uchumi, culture na mazingira yetu tumejijengea asilia ya kutegemea kila kitu toka kwa wengine, wazungu, na hivyo hatujatambua kuwa kila kitu kinatoka kwetu na kuwa responsible wa hali yetu halisi. Tujifunze kutokana na makosa yetu, na ya wengine ili tuweze kuishi maisha bora, tuwachie watoto wetu mazingira na misingi bora ya maisha, na sio mifarakano na madeni kama walivyotuachia wengi wa mababu zetu. Wenzetu walioendelea waacha misingi bora na mali, mali kama material haridhiwi rafiki yangu, ila mali kama mali na namna ya kuendeleza mali na kuiridhisha kwenye kizazi kijacho ndio inayoridhiwa. Mali ya kuridhiwa peke yake, bila namna ya kuendeleza mali siku zote inagonga mwamba kwani mwenye mali alishaondoka, na anayemiliki mali hajui namna ya kuiendeleza. Na hii ndio hali halisi ya matajiri wa kiafrica, mwenye mali akifa na mali inakufa. Wenzetu wazungu, mwenye mali akifa mali inabakia na kuridhishwa kizazi na kizazi, kwanini sisi hatufanyi hivyo kwasababu ya tamaduni duni na culture ya kuwa tegemezi, mali haiendani na akili tegemezi. Mali inaendana na akili huru, na hali huria.
 

The Fatherhood Life Reader(s) Signature and Disclaimer. Content of this Blog (The Fatherhood Life) is intended for the use of reader(s) only and may contain privileged, confidential, or proprietary information that is exempt from disclosure under law. Reader(s) discretion is required. If you have received this link in error, please inform us promptly by profile e-mail, and then exit the link immediately. Content of this blog are protected under the privacy, 1st amendment and private property laws. Do not distribute, print, download and or copy content of this Blog without Blog administrator’s permission. Thank you and may God bless you and The United States Of America. "In God we Trust"

No comments: