Thursday, December 9, 2010

Happy Belated Birthday Tanzania/Tanganyika, The Pride Of Africa

Eee!!!! Jana ndio huku leo) ndio Uhuru sio. Birthday ya mwana Tanzania sio. Happy Birthday Tanganyika, ndio uzee tena hivyo. Nderemo na vifijo, ila wanasiasa porojo lukuki utendaji hewa kazi kuiba, rushwa na kumkandamiza mwanachi. Tunahitaji viongozi Africa. Hii siasa ya sera chama tawala/viongozi kufanya mapendekezo yao tuu kuwa sheria na mapendekezo ya wataalamu kama hwayataki kuwa kinyime cha sheria, inatupotosha africa na ni lazima tuache kujidangaya maanake ukweli siku zote ni ukweli hata kama ni mchungu kama sifongo sio. Angalia Zimbabwe, 1999 ilikua almost first class African country leo, masikini zaidi ya Congo. Sera za kujilinda na kukataa ukweli na mapendekezo ya wataaluma. Karibu nchi zote za Africa zinapiga hatua tatu mbele na kurudi hatua 6 nyuma. Tunahitaji viongozi. Kiongozi ni mtu anayeweza kubadili mwelekeo, kutumia ujuzi/wajuzi, taaluma/wanataaluma, tekinolijia/wanatekinolojia na mali/wenye mali ili kuboresha ustawi wa jamiii na kuleta maendeleo katika jamii kwa ujumla. Saasa kam hadi leo tuna mgao wa umeme, elimu duni, uzalishaji duni, maji hakuna, barabara hewa, hata tujidangaye vipi maendeleo ni hewa. Maana vitu hivi hivyo ndivyo vyobmo nguzo na misingi mama ya maendeleo. Africa tuanche kujenga Ghorofa kwenye msingi wa matope maana ghorofa litaporomoka. Tuanze kujenga misingi ya magorofa yetu kwnye Zege imara na lenye nondo za kutosha, na maghorofa yetu yatasimama imara na timilifu. Huu ni wosia wangu, Mtanzania/Mwafrica atajikomboa mwenyewe na sio mtu mwingine atakayemkomboa, maanake "wawezamlazimisha punda kwenda mferejini lakini huwezi mlazimisha Punda huyo kunywa maji". Tukumbuke kuwa kuna "utumwa wa nguvu kazi na utumwa wa kimafikara/kisaikolojia". Tusiwe watumwa wa mafikara/kisaikolojia kuwa hatuweze kujikomboa au kuboresha maisha yetu maanake twaze, ila nia na uongozi imara ni duni. WOSIA WANGU KWA SIKU HII YA KUZALIWA KWA TAIFA LA TANZANIA/TANGANYIKA. AFRIKA OYEE!!!! TANZANIA!!!!!!!

No comments: